IPTL/PAP ya wekeza katika mapambano dhidi ya Malaria

IPTL/PAP ya wekeza katika mapambano dhidi ya Malaria

6-001

Mama huyu na mtoto wake aliye chini ya miaka 5 ni miongoni mwa watu waliopo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa Malaria wasipotumia vyandarua vyenye viwatilifu. Mama huyu ni miongoni mwa wananchi walionufaika na msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu uliotolewa na IPTL/PAP kwa wakazi wa Wazo na Kunduchi.

25 Aprili 2015: Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya Pan Africa Power Solutions (T) Limited imetoa msaada wa vyandarua 700 vyenye viwatilifu kwa vituo vya afya vilivyopo kwenye kata za Wazo,  Kunduchi na Kawe kwenye wilaya ya Kinondoni katika kuadhimisha ya siku ya Malaria duniani.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa IPTL na PAP, Katibu na mshauri mkuu wa sheria wa kampuni hizo, Bw. Joseph Makandege alisema: “IPTL inakubaliana kabisa na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Malaria Duniani inayosema, Wekeza katika mapambano dhidi ya Malaria sisi kama IPTL/PAP tunaamini kuwa kuwekeza katika mapambano dhidi ya malaria kunabaki kuwa ‘nyenzo kubwa’ katika afya duniani kwa sababu kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kunaongeza upatikanaji wa rasilimali watu.”

Sambamba na msaada huo wa vyandarua pia kampuni ya IPTL imetoa elimu kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo na wakazi wa maeneo ya Kunduchi kuhusiana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na namna unavyoambukizwa, njia za kujikinga na matibabu sahihi ya ugonjwa huo.

“Kwa niaba ya Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Makampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), BW. Harbinder Singh Sethi na kwa niaba ya Menejimenti, IPTL/PAP leo inatoa vyandarua 700 ambavyo vitagawiwa vituo vyote vya afya katika kata za Wazo na Kunduchi, vikiwa ni vituo vinavyozunguka mitambo yetu ya kufua umeme iliyopo Sala Sala karibu na Tegeta,” Aliongezea Bw. Makandege.

Msaada huo ambao umelenga kuwanufaisha wagonjwa wanaolazwa, wanopumzishwa, kina mama wajawazito, na kina mama wanaojifungua katika vituo vya afya vya kata ya Wazo na Kunduchi.

Malaria ni tatizo kubwa la afya nchini Tanzania, ambapo takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa Malaria inachangia vifo vya kila mwaka vya kadri ya watu 60 elfu, huku asilimia 80 ya vifo hivyo huwapata watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

“Takwimu hizi si nzuri katika uhai wa uchumi wa nchi yetu. Hivyo basi, kila mtu hana budi kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake katika kutokomeza Malaria hapa nchini. Sisi kama kampuni ya IPTL/PAP tumeanza. Hatutarudi nyuma. Tutakuwa bega kwa bega na serikali katika mapambano haya,” Alisisitiza Bw. Makandege

Bodi ya IPTL, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Bwana Harbinder Singh Sethi, imeamua kujikita katika Nyanja za Afya, Michezo na Elimu katika awamu yake ya kwanza ya utekelezaji wa programu yake ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii – Corporate Social Responsibility – CSR (Soma Zaidi)

 

 

No Comments

Sorry, the comment form is closed at this time.